Wakala wa mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Sadio Mane amekanusha tetesi kuhusu sababu ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal kuhama klabu ya Liverpool kuwa tatizo halikuwa mshahara mdogo ambao alikuwa analipwa kwenye klabu hiyo.

Baada ya sadio mane kuhamia klabu ya Bayern Munich, kuna taarifa zimekuwa zikisambaa sana mtandaoni ambapo baadhi ya waandishi wamekuwa wakidai kuwa mshahara kuwa chini ni moja ya sababu yeye kuikacha klabu hiyo, huku wengine wakidai kuwa ameondoka  kwa sababu ya kimikataba.

Sadio Mane

Bacary Cisse wakala wa Sadio Mane amesafisha uvumi huo kwa kuweka wazi, wakati akiwa anahojiwa na kituoa cha TV5Monde alinukuliwa akisema, “zote hizo ni tetesi za uongo. 

“Hatukutaka kuzungumzia hilo. Mchezaji aina ya Sadio Mane hawezi kupokea mshahara ambao watu wanauzungumzia. Kiasi kinachosemwa mtandaoni ni uongo kabisa.

“Sadio alikuwa tayari anapokea zaidi alipojiunga na Liverpool akitokea Southampton. Alipoongeza mkataba mwaka 2018 mshahara wake ulikuwa mkubwa kuliko kiasi ambacho kinatangazwa kwenye vyombo vya habari.”


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa