Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na PSG Thomas Tuchel anatarajiwa kuanza majukumu yake ndani ya klabu ya Bayern Munich baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo masaa machache yajayo.

Kocha Thomas Tuchel anatarajiwa kua kocha mkuu wa klabu ya Bayern Munich baada ya aliyekua kocha wa klabu hiyo Julian Nagelsman kufukuzwa kazi ndani ya timu hiyo, Hivyo Bayern kocha pekee ambaye wameona atawafaa ni kocha huyo wa zamani wa Chelsea.TuchelJulian Nagelsman ametimuliwa ndani ya klabu ya Bayern Munich baada ya mwenendo mbaya katika ligi kuu ya Ujerumani, Huku klabu ya Borussia Dortmund ikiwa vinara wa ligi kuu ya Ujerumani wakiwaacha klabu ya Bayern Munich kitendo ambacho kinaelezwa hakijawafurahisha mabosi wa klabu hiyo.

Kocha Thomas Tuchel anatarajiwa kusaini kandarasi ya kuitumikia klabu ya Bayern Munich masaa machache yajayo na kibarua chake rasmi atakianza rasmi siku ya jumatatu akiongoza mazoezi ya klabu hiyo, Huku wachezaji wengi wakiwa kwenye timu zao za taifa.TuchelTuchel ana kibarua cha kutwaa mataji mawili ambayo ni taji la ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, pamoja na taji la ligi ya mabingwa ulaya ambapo atacheza mchezo wa robo fainali wa michuano hiyo dhidi ya klabu ya Manchester City mapema mwezi April.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa