Werner Kukikosa Kombe la Dunia

Mshambuliaji wa RB Leipzig na timu ya Taifa ya Ujerumani Timo Werner, atakosekana kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.

 

Werner Kukikosa Kombe la Dunia

Mshambuliaji huyo wa Ujerumani Timo Werner hatashiriki Kombe la Dunia baada ya kupata jeraha kwenye kifundo cha mguu alipokuwa akiichezea RB Leipzig katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk uliomalizika kwa RB kushinda kwa mabao 4-0.

Werner aliumia katika kipindi cha kwanza baada ya kuchezewa vibaya na Taras Stepanenko wa Shakhtar Donetsk, na alitolewa nje baada ya kuonekana kushindwa kuendelea kwenye mchezo huo.

Werner Kukikosa Kombe la Dunia

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alibadilishwa na Emil Forsberg dakika ya 19 na Leipzig timu hiyo kujihakikishia kutinga hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi F.

Klabu hiyo ilitangaza hapo jana kuwa Werner hatacheza tena mwaka huu. “Timo Werner alipata jeraha la kifundo cha mguu jana usiku katika ushindi dhidi ya Shakhatar Donetsk na atakuwa nje kwa mwaka huu wa 2022”

Tangu aanze kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2017, Werner amefunga mabao 24 katika mechi 55 za nchi yake.  Na alijiunga tena na Leipzig mnamo Agosti baada ya misimu miwili na Chelsea na kufunga mabao tisa katika mechi 16 za klabu hiyo ya Bundesliga, lakini hatapanda ndege kwenda Qatar.

Werner Kukikosa Kombe la Dunia

Habari hizi ni pigo kwa kocha mkuu wa Ujerumani Hansi Flick anapojiandaa kwa mchuano wake wa kwanza mkubwa tangu achukue nafasi ya Joachim Low, na mchezo wao wa ufunguzi watacheza  dhidi ya Japan Novemba 23.

Acha ujumbe