Kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen ya Ujerumani raia wa kimataifa wa Hispania Xabi Alonso ameendelea kupiga kazi iliyotukuka ndani ya klabu hiyo inayoshikriki ligi kuu ya Ujerumani.
Bayern Leverkusen imekua kwenye kiwango bora sana msimu ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa, Huku wakiwa vinara wa ligi kuu ya Ujerumani mpaka sasa.Xabi Alonso amefanikiwa kuiongoza klabu hiyo mechi 14 mpaka sasa ndani ya msimu huu, akifanikiwa kushinda michezo 13 mpaka sasa na kusuluhu mchezo mmoja wakiwa hawajapokea kipigo bado msimu huu.
Klabu ya Bayern Leverkusen inaonekana ni klabu ambayo inaweza kuleta ushindani mkubwa kwa Bayern Munich msimu, Hii inatokana na mwenendo wa timu hiyo mpaka sasa na matokeo ambayo wanayapata kwenye michuano yote.Klabu ya Bayern Leverkusen chini ya Xabi Alonso pia imefanikiwa kuweka rekodi kwenye ligi tano barani ulaya, Ambapo kwenye mechi 14 tu ambaz timu hiyo imecheza imeshafanikiwa kufunga mabao 51 ikiwa ni idadi kubwa kuliko timu yeyote kwenye ligi tano bora barani ulaya.