Xabi Alonso Aendelea Kuishangaza Ulaya

Gwiji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Liverpool, na Bayern Munich Xabi Alonso ambaye kwasasa ni kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen ameendelea kuishangaza ulaya.

Xabi Alonso anaendelea kufanya maajabu ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen kwani mpaka sasa amefanikiwa kuiongoza klabu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya alama tano.xabi alonsoKocha huyo ambaye alichukua timu hiyo katikati mwa msimu uliomalizika na kufanikiwa kuifanya klabu hiyo kua moja ya timu tishio kunako ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Kocha Xabi Alonso anaonekana anaweza kuondoa utawala wa klabu ya Bayern Munich msimu huu kunako ligi kuu ya Ujerumani, Kwani mpaka sasa yupo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo akiongoza kwa alama tano tena baada ya kufanikiwa kuifunga Bayern Munich siku ya jumamosi.xabi alonsoMpaka sasa kocha Xabi Alonso amefanikiwa kuiongoza Bayern Leverkusen katika michezo 31 msimu huu, Huku akiwa hajapoteza mchezo hata mmoja akiwa ameshinda michezo 27 na kusare michezo minne Bayern Leverkusen ikiwa klabu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika ligi kubwa tano barani ulaya.

Acha ujumbe