Timu ya Manchester City imefanikiwa kuchukua kombe la Carabao Cup jana baada ya ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Hii ilikuwa ni mechi nzuri sana kwa Manchester City ambao walionekana kushambulia lango la Spurs kama nyuki. Toka dakika ya kwanza mpaka mwisho City walionekana wakitamani kunyanyua kombe hilo kwa mara nyingine tena.

Timu hiyo ilikuwa bora sana katika eneo la kiungo pamoja na ulinzi ambapo viungo wakabaji Gundogan na Fernandinho walikuwa bora sana, huku wale viungo washambuliaji De Bruyne, Sterling na Mahrez wakiwa mwiba mkali kwa walinzi wa Tottenham.

Alikuwa ni Laporte aliyeamua matokeo hayo kwa kichwa akimalizia mpira uliokufa aliopiga De Bruyne. Kati ya mashuti 21 waliyopiga City ni manne tu ndiyo yaliyolenga lango la Spurs. Hii inaonesha namna ambavyo bado safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao inamkosa mtu kama Aguero.

Fainali ya Carabao Cup ilifanyika katika uwanja wa Wembley na kushuhudiwa na mashabiki 8000 kama mwanga wa kuanza kuruhusu watazamaji kurudi uwanjani.

City sasa wanachukua kombe hilo kwa mara ya nne mfulululizo toka waanze kufanya hivyo mwaka 2018 wakiwa chini ya Pep Guardiola.

Manchester City inashika nafasi ya kwanza kwenye EPL na ipo katika nusu fainali ya UEFA ambapo itakutana na PSG, je, watafanikiwa kuchukua makombe hayo mawili yaliyobaki?


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

CHEZA HAPA

 

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa