Klabu ya Manchester United imefanikiwa kutwaa taji la michuano ya Carabao Cup baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Newcastle United kwa jumla mabao mawili kwa bila katika mchezo uliopigwa katika dimba la Wembley.

Carlos Casemiro alifanikiwa kupachika bao la kwanza dakika ya 33 ya mchezo kabla ya Marcus Rashford kufunga bao la pili mnamo dakika ya 39 ya mchezo, Kupitia mabao hayo yalisaidia kuhakikisha klabu ya Manchester United wanatwaa taji la michuano ya Carabao.manchester unitedMashetani wekundu sasa ni rasmi wameumaliza ukame wa miaka sita bila kutwaa taji lolote baada ya kuichabanga klabu ya Newcastle na kufanikiwa kutwaa taji la Carabao, Huku klabu hiyo ikisalia katika michuano yote mitatu ikiwa na uwezekano pia wa kutwaa mataji hayo.

Kocha wa klabu ya Man United Erik Ten Hag anakua kocha wa kwanza kuipatia taji klabu ya Manchester United tangu mwaka 2017 Jose Mourinho alipofanya hivo, Kocha huyo amefanikiwa kuijenga timu hiyo kwa muda mfupi na kuonesha mabadiliko makubwa.manchester unitedMarcus Rashford yeye anaendelea kua na msimumzuri ndani ya klabu ya Manchester United akiwa ameshafunga mabao 25 mpaka sasa kwenye michuano yote kwenye michezo 38 aliyocheza mpaka sasa, Mshambuliaji huyo anaendelea kuuthibitishia ulimwengu ubora wake sio wa kubahatisha.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa