Scott Carson ameweka historia mpya ndani ya Ligi ya Mabingwa kwa kuwa golikipa ambaye hajacheza mechi nyingi zaidi katika historia ya UCL.
Mlinda lango huyo wa Manchester City Carson, 36, ambaye ni chaguo la tatu nyuma ya Ederson na Zack Steffen aliingia kama mbadala wa Ederson kipindi cha pili, akicheza tena kwenye mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2005 alipoichezea Liverpool akiwa na umri wa miaka 19.
Man City waliibomoa Sporting CP kwa mabao 5-0 mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora mwezi uliyopita lakini walikwenda sare ya bila kufungana siku ya Jumatano katika dimba la Etihad Stadium.
“Scott ni muhimu sana,” meneja wa City Pep Guardiola alisema baada ya mchezo huo.
“Sababu ni chemistry katika chumba cha kubadilishia nguo na Eddie na Zack. Watu wanamsikiliza wakati anazungumza na aliokoa mchomo mkubwa kwenye mchezo.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.



