Ceferin: Liverpool Watashinda Ligi Kuu

Raisi wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema haoni uwezekano wa Liverpool kumaliza msimu bila kuwa mabingwa wa Ligi Kuu.

Ceferin wanauhakika wa kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu kama utaendelea lakini kwasababu ya Corona mechi zimehairishwa hivyo wanazubiri uamuzi wakusubiri au kufanya msimu wa 2019/2020 batili.

Jurgen Klopp anatofauti ya alama 25 na nafasi ya Manchester City na huku ikiwa bado michezo 8.

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia moja ya magoli.

“Sioni kama Liverpool watakosa taji. Kama Ligi zikiendelea, lazima watashinda. Sisa uhakika sana kama watashinda lakini inaonekana watashinda” amesema Ceferin

“Najua mashabiki watahuzunika kama mechi zitachezwa bila mashabiki, lakini naamini watashinda iwe kwa namna moja au nyingine.”

Ceferin amesema anaamini ligi za Italia na Hispania zitaendelea, nchi hizo za Ulaya zimeathiriwa sana na virusi vya Corona.

2 Komentara

    Liver ubingwa wao msimu huu.

    Jibu

    Najua mashabiki watahuzunika kama mechi zitachezwa bila mashabiki, lakini naamini watashinda iwe kwa namna moja au nyingine.”

    Jibu

Acha ujumbe