Mchezaji wa Villarreal ambaye yupo kwa mkopo Valencia, Denis Cheryshev yupo chini ya uchunguzi kufuatia madai ya matumizi ya madawa kinyume na taratibu.

Staa huyu aliwafungia Urusi magoli 4 wakati wa fainali za Kombe la Dunia. Uchunguzi dhidi ya staa huyu unafuatia kutiliwa shaka baada ya baba yake kusema kuwa alitumia matibabu ya dawa za homoni za ukuaji ikitambuliwa kitaalamu kama Human Growth Homone (HGH).

Taasisi ya kuzuia matumizi ya madawa duniani (World Anti-Doping Agency) inaripoti kwa ishu hiyo iko chini ya mamlaka za kuzuia matumizi ya madawa ya taifa la Uhispania. Denis amecheza gemu 5 katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia huku wao wakiwa wenyeji wa mashindano hayo.

Matumizi ya madawa ya HGH pekee bila ushauri wa kitabibu yanaweza kumfanya mkali huyu akapewa adhabu ya kutojihusisha na soka kwa miaka minne ikiwa atathibitika kutumia.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa