Robert Lewandowski ataikosa mechi ya nusu fainali ya kwanza ya Copa de Rey ya Barcelona dhidi ya Real Madrid Alhamisi kutokana na jeraha la misuli ya paja.
Barca leo hii imefichua wazi kuwa Lewandowski amepata mkazo wa msuli wa paja lake la kushoto.
Vinara hao wa ligi wamesema kwamba mshambuliaji huyo mahiri kupona kwake kutaamua kupatikana kwake siku tatu kabla ya mchuano mwingine wa Clasico huko Santiago Bernabeu.
Jeraha la Lewandowski ni pigo lingine kwa Xavi baada ya kushindwa kwa 1-0 na Almeria siku ya jana huku hicho kikikuwa ni kipigo cha pili tu cha LaLiga msimu huu kwa wababe hao wa Catalan, ambao wapo mbele ya Madrid kwa pointi saba kileleni.
Barca pia walipata pigo la kutupwa nje ya Ligi ya Europa na Manchester United wiki iliyopita, na kupoteza mchezo wa marudiano Old Trafford 2-1 baada ya Lewandowski kufunga bao la 25 msimu huu.
Kikosi cha Xavi kitamenyana na Los Blancos huko Camp Nou kwenye LaLiga mnamo Machi 19 baada ya kumenyana na Valencia na Athletic Bilbao. Mechi ya pili ya nusu fainali ya Copa itafanyika Aprili 5.