Dau la Kumtoa Neymar PSG Liko Wazi?

Haijawa mda mrefu toka Neymar achukuliwe na klabu ya PSG inayoshiriki Ligi 1, ni mwaka 2017 tu alipoenda huko. Nyota huyu alitoka Barcelona na PSG kwa dau linalotajwa kuwa paundi milioni 222, dau kubwa zaidi kuwahi kulipwa kwa mchezaji kwenye ulimwengu wa soka. Dau hili lilikuwa ni dau la kununua mkataba (Relese Clause)!

Maisha ya Neymar baada ya kuchukuliwa kwa dau kubwa!

Msimu wake wa kwanza tu klabuni PSG, Mbrazili huyu amefanikiwa kushinda mataji yote ya matatu ya ndani ya Ufaransa.

Walishinda Ligue 1, Coupe de France, Coupe de la Ligue, pia akanyakua tuzo binafsi kama mchezaji wa mwaka wa Ligue 1.

Amefunga magoli 19 na asisti 13 kwenye Ligue 1. Pia, amechapa magoli 6 na asisti 3 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, nyota huyu ameripotiwa kutofurahia maisha yake klabuni hapo akiwa na nia ya kutaka kurejea tena La Liga. Licha ya kuhusishwa na klabu ya Real Madrid, anadaiwa mapenzi yake bado yapo Barcelona na huenda akarejea huko.

Inakuwaje kumtoa PSG

Kwa sasa dau la kumtoa nyota huyu halipo wazi rasmi wakati nyota huyu akiwa anatamani kusepa. AS wanaripoti kuwa Neymar hana sharti la kununuliwa mkataba kwenye mkataba wake wa sasa, isipokuwa anaweza akanunuliwa kwa dau la kati ya paundi milioni 160 kwenye msimu wa mwaka 2020.

Makala iliyopita

Acha ujumbe