De Gea Kulipwa Zaidi United

Manchester United wanaripotiwsa kuwa wanafanya kila wawezalo kuongeza mkataba wa mlinda mlango wao David De Gea. Mkataba wa nyota huyu unaisha mwezi Juni mwakani, itakuwa hasara kubwa kwa klabu hii kumpoteza nyota huyu bure akiwa mchezaji huru.

Calciomercato wanaripoti kuwa Man Utd wako tayari kumfanya nyota huyu kuwa mchezaji anayelipwa dau kubwa zaidi klabuni hapo katika kutengeneza mazingira ya nyota huyu kusaini mkataba mpya.

Nyanda huyu alijiunga na Manchester United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid na amekuwa sehemu muhimu ya klabu hiyo. Kwa kipindi cha miaka 7 klabuni hapo, nyota huyu mwenye miaka 27 amecheza jumla ya gemu 325.

Lakini pia, kwa uzoefu na uwezo wake amekuwa golia namba 1 katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, akianza kucheza mwaka 2014 na amecheza gemu 36 mbaka sasa na alikuwa golia aliyeanza katika gemu za kimataifa za michuano mikubwa miwili iliyopita.

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe