Dondoo za Usajili: Fabregas, Cahill

Bayern Munich Kuweka bunda mezani kwa Callum Hudson-Odoi

Bayern Munich wanaripotiwa kuwa tayari kutenga bunda la paundi milioni 13 kumsajili kinda wa chelsea anayecheza nafasi ya kiungo Callum Hudson-Odoi kwa mujibu wa Daily Mail. Nyota huyu anatazamiwa kuwa mmoja wa viungo bora sana siku za usoni japokuwa amechexza gemu yake moja tu ya Ligi Kuu Uingereza msimu huu.

Safari ya Gary Cahill kwenda Aston Villa imekwama!

Kwa mujibu wa Daily Telegragh, Aston Villa wameamua kujiondoa kwenye mbio za kumsajili Gary Cahill kutokaΒ  Chelsea. Sababu inadaiwa kuwa gharama iliyopo kumnasa nyota huyu. Villa walikuwa na mpango wa kumsajili nyota huyu ambaye alishawahi kuitumikia klabu hiyo lakini imebanika kuwa hata wakimtaka kwaΒ  miezi 6 tu itawagharimu hadi paundi milioni 4 kwa ajili ya mshahara na ada.

Hatma ya Fabregas Chelsea

Fabregas atakuwa huru kuzungumza na klabu zingine kuanzia mwezi Januari. Kwa mujibu wa jarida la kihispania la Marca, nyota huyu amesema anasepa Chelsea mkataba wake unapoisha mwisho wa msimu huu. Hata hivyo, meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amesema anahitaji nyota huyu asalie klabuni hapo.

Meneja wa Juventus kwenda United

Kwa mujibu wa calciomercato, bosi wa Juventus bwana Massimiliano Allegri alikuwa akihusishwa na kibarua cha umeneja cha Manchester United. Lakini meneja huyu akizungumza na vyombo vya habari amesema kwa sasa bado ana mkataba na Juventus na anafurahia kuwepo hapo.

Modric achomoa ofa ya mkataba mpya Real Madrid.

Kwa mujibu wa ripoti ya Telemadrid kupitia AS, nyota wa klabu hiyo mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2018 Luka Modric amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid akiripotiwa kuwa anahitaji kusepa klabuni hapo. Nyota huyu anahusishwa na klabu ya Inter Milan.

Brahim Diaz Kusepa Manchester City

Kiungo wa Manchester City, Brahim Diaz anaripotiwa yupo mbioni kusepa klabuni hapo na kujiunga na Real Madrid kwa dau la paundi milioni 13.5. Kinda huyu anatarajia kutia wino dili la kuwepo Real Madrid kwa misimu sita ijayo.

3 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habar njema sana πŸ‘

    Jibu

    Makal nzur

    Jibu

Acha ujumbe