Andrey Santos Amalizana na Chelsea kwa uhamisho wa £11m

Chelsea wanatarajiwa kuwa moja ya timu zenye shughuli nyingi zaidi za Premier League kwenye dirisha la usajili la Januari ikiwa tayari imepata dili la kumnunua mshambuliaji wa Molde David Datro Fofana.


Chelsea wamemalizana na kiungo chipukizi na mahiri Andrey Santos kutoka Vasco da Gama. Mbrazil huyo amepigwa picha jijini London akisherehekea mwaka mpya huku akijiandaa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kuhamia Stamford Bridge.

 

Andrey Santos

Todd Boehly anatarajiwa kumuunga mkono Graham Potter na idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha la usajili la Januari. kwa mujibu wa football.london inaeleza kuwa The Blues wako sokoni kutafuta mshambuliaji, kiungo wa kati, beki wa kati na chaguo la kumnasa Reece James.

David Datro Fofana tayari amesajiliwa na The Blues wakati dirisha la usajili likifunguliwa rasmi, ingawa fowadi huyo wa Ivory Coast anatarajiwa kuondoka kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Boehly anaendelea na mtindo wake wa kusajili vijana wenye vipaji huku akikaribia kupata dili kwa Santos.

 

Andrey Santos

Andrey Santos alipigwa picha akisherehekea Krismasi kwenye viwanja vya Chelsea kwani mapambo yake yote yalikuwa ya buluu na nyeupe, akidokeza kwamba uhamisho ulikuwa karibu.

Jarida la Ufaransa la Le10 Sport liliandika mwezi uliopita kwamba Chelsea walikuwa tayari kukubaliana na Santos kwa kitita cha paundi milioni 15, huku The Blues wakisonga mbele haraka kuinasa saini yake kabla ya kwenda kwingineko.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, The Blues watalipa ada maalum ya €12.5million (£11million) kwa Santos ambaye anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wa kimatibabu siku zijazo baada ya makubaliano ya uhamisho wake kufikiwa.


Kinda huyo ameshiriki katika kila ngazi ya vijana kwa Brazil na kuna uwezekano ni kwamba atashiriki katika timu ya wakubwa katika miaka ijayo.

Kuwasili kwa Andrey Santos kungefuatia mastaa kama Carney Chukwuemeka, Cesare Casadei, Gabriel Slonina na Fofana, ambapo Boehly anaendelea kutambua na kusajili vijana wenye vipaji kutoka kote ulimwenguni kama sehemu ya maono yake ya muda mrefu huko Stamford Bridge.

Acha ujumbe