Baada ya Kutwaa Ubingwa wa Kombe la Dunia Mac Allister Aongezewa Majukumu Mazito Brighton

Kocha wa Brighton Roberto De Zerbi amemuunga mkono mshindi wa Kombe la Dunia Alexis Mac Allister kukabiliana na umaarufu wake mpya alioupata duniani.

 

Mac Allister

Alexis Mac Allister atakuwa kitovu cha umakini na matarajio zaidi kuliko hapo awali baada ya kuisaidia Argentina kushinda dhahabu nchini Qatar.

Lakini kocha mkuu De Zerbi alisema: “Nafikiri anatakiwa kufurahia tu. Ili kucheza kama alivyofanya hapo awali.

“Ni ngumu kwa hakika lakini ni bora ikiwa umeshinda Kombe la Dunia, ni hatua moja zaidi, sio hatua moja chini.

“Kwa hili, lazima atulie, afurahie, na atusaidie lakini lazima tumsaidie. Nilizungumza juu ya familia, juu ya nyumbani, kwa sababu hii.Lakini yeye ni mtu mzuri, mtu mwenye akili. Amekomaa.”

Mac Allister alikuwa na wafuasi wapatao 350,000 wa Instagram kipindi akienda kushiriki Kombe la Dunia. Idadi hiyo imeongezeka hadi karibu milioni 3.5.

Mashabiki wake wengi watamtarajia kuondoka Albion lakini De Zerbi amemshauri abaki hadi angalau mwisho wa msimu.

 

Roberto De Zerbi

Alisema: “Kuanza tena baada ya kushinda Kombe la Dunia si rahisi sana.

“Mechi ya mwisho kucheza ilikuwa fainali ya Kombe la Dunia.

“Kwake, Brighton ni nyumbani kwake na kucheza miezi sita nyingine nyumbani ni muhimu sana kwake katika wakati huu.

“Sipendi kuwa mbinafsi, kwa sababu sipendi kufanya hivyo na wachezaji wangu.

“Lakini ikiwa naweza kumpa pendekezo basi lazima nimwambie ninachofikiria. Nilizungumza naye na kumueleza.”

De Zerbi alisema Mac Allister yuko tayari kiakili kucheza dhidi ya Everton usiku wa leo lakini hali yake ya kimwili itapimwa leo. Bashiri na kitochi au bila bando mechi hii, Bonyeza hapa kutazama ODDS kubwa na bomba kupitia machaguo spesho ya meridianbet ili kuingia mchezoni.

Aliongeza: “Tuna furaha kwake na kwetu ni mchezaji muhimu sana. Ni bora kucheza na Alexis kuliko bila yeye.”

Acha ujumbe