Klabu ya Soka ya Chelsea imejikuta ikambulia kipigo kizito dhidi ya klabu ya Brighton Hove and Albion. Klabu hiyo imefungwa magoli manne kwa kwa moja katika mcheso uliopigwa katika dimba la The American Express Community.

Baada ya klabu ya Chelsea kupoteza mchezo huo unakua mchezo wa kwanza kwa kocha wa klabu hiyo Graham Potter kupoteza tangu apewe majukumu ya kuinoa klabu hiyo kutoka jiji la London.chelseaBrighton chini ya mwalimu Roberto de Zerbi walionekana kua wagumu sana kufunguka na wakiwa wazuri zaidi kwenye mipira ya kushtukiza na kuweza kupata mabao manne katika mchezo huo. Mabao ya Brighton yalifungwa na Leandro Trossard, magoli mawili ya kujifunga kutoka kwa Loftus cheek pamoja na Trevoh Chalobah pamoja na Pascal Gross huku bao pekee la Chelsea likifungwa na Kai Harvetz.

Katika michezo mingine klabu ya Tottenham Hotspurs walifanikiwa kupindua meza baada ya kutanguliwa kwa mabao mawili kwa bila na kufanikiwa kushinda mabao matatu kwa moja. Magoli ya Spurs yalifungwa na Ryan Ssegnon, Ben Davies, na goli la ushindi likifungwa na Rodrigo Bentacur huku magoli ya utangulizi ya Bournemouth yakifunfwa na Kieffer Moore.chelseaKlabu ya Newcastle wakiwa kwenye ubora wa hali ya juu kabisa wamefanikiwa kushinda ushindi mnono wa mabao manne kwa bila dhidi ya Aston Villa. Mchezo huo uliopigwa katika dimba la St. James Park ulishuhudua Newcastle wakitawala katika kila eneo katika mchezo huo, Huku magoli yao yakifungwa na Callum wilson aliefunga mabao mawili, kabla ya mbrazil Joelinton kufunga bao la tatu na Miguel Almiron kukamilisha karamu ya mabao.

Klabu ya Newcatle inakweea hadi nafasi ya nne wakiwa na alama 24 huku klabu ya Tottenham wao wakiendelea kubaki nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 26, Wakati huo wakiwa wamecheza michezo 13 wakiwa wamewatangulia Chelsea na Man United kwa mchezo mmoja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa