Manchester City watamtathmini Erling Haaland kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester City baada ya kushindwa kuendelea na kutolewa nje kwenye mechi dhidi ya Borussia Dortmund katikati ya wiki.

 

City Kutathmini Hali ya Haaland Kabla ya Pambano na Leicester

Kurudi kwa Haaland kwenye timu yake ya zamani pale katika kiwanja cha Signal Iduna kulimalizika mapema Jumatano kwa sababu ya homa na kupata jeraha na  City hawana uhakika kama watakuwa naye hapo kesho.

City watasafiri kumenyana dhidi ya Leicester City katika mechi ya mapema hapo kesho kwa mchezo ambao  ambao unawapa nafasi ya kuweka presha  kwa Arsenal, ambao watawakaribisha Nottingham Forest hapo Jumapili huku tofauti yao ikiwa ni alama 1 pekee.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya ziara hiyo ya King Power Stadium, kocha mkuu wa City,  Pep Guardiola amesema kuhusu mshambuliaji wake; “Anajisikia vizuri lakini tutafanya mazoezi leo na tutatathmini baada ya saa chache na tutamuona anavyojisikia kisha tutaamua.”

City Kutathmini Hali ya Haaland Kabla ya Pambano na Leicester

Haaland ameanza msimu vizuri ndani ya Primia Ligi baada ya kutoka Dortmund, huku akifunga 17 katika mechi 11 za Primia Ligi msimu huu, tayari ni wa pili pamoja na mchezaji wa Norway katika kampeni moja ambayo Ole Gunnar Solskjaer, alifunga mabao 18 mnamo 1996-97.  Mabao yake yamekuwa yenye thamani ya pointi 11, nyingi zaidi kwa mchezaji wa Pep katika kampeni moja tangu Raheem Sterling afanye hivyo mnamo 2017-18.

Iwapo hatoweza kucheza dhidi ya Leicester, Julian Alvarez anaweza kuchukua nafasi yake katikati mwa washambuliaji. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga mara mbili katika mechi tisa za ligi akiwa na klabu ambapo ameanza mechi moja pekee.

City Kutathmini Hali ya Haaland Kabla ya Pambano na Leicester

Licha ya muda wake mdogo kwenye kikosi cha kwanza cha  Guardiola ana imani kamili na uwezo wa Alvarez kuziba pengo

“Ikiwa Haaland hatacheza, basi Alvarez ndiye atachukua nafasi yake. Simhukumu Julian kuhusu mabao mangapi amefunga, akicheza dakika 90 kila mchezo atafunga.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa