Declan Rice Nje Mwezi 1!

Kiungo tegemezi wa West Ham United, Declan Rice atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kufuatia kupata jeraha la goti. 

Rice alikuwa kwneye majukumu ya kitaifa ya timu ya Uingereza kiacheza dakika tisa katika mechi mbili za mwanzo dhidi ya Albania na Poland, kabla ya kupata majeraha.

Declan Rice
Ameanza Michezo Miwili Kati Ya Mitatu Ya Uingereza

Akichezea West Ham, Declan amefananishwa kufanya kazi moja sawa na Fabinho wa Liverpool na N’golo Kante wa Chelsea. Kuumia kwake ni pigo kubwa sana kwa West Ham United ambao wamekuwa kwenye kiwango kizuri msimu wakishinda michezo 14 kati ya 29.

West Ham United wanashika nafasi ya saba wakiwa na alama 49 sawa na Liverpool na Totenham huku wapo mchezo mmoja nyuma. West Ham watashuka dimbani leo kucheza na Wolves na endapo watashinda mchezo huu watapanda mpaka nafasi ya nne. West Ham wamekuwa wakipambania kubaki nafasi nne za juu kwenye Premier League ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki UEFA Champions League msimu ujao.

Kocha wa West Ham United, David Moyes atalazimika kumuanzisha nahodha wake Miko Noble kuanza nafasi ya Rice katika mechi ya leo. Rice amekuwa mchezaji muhimu katika timu ya taifa ya Uingereza na Kocha Gareth Southgate atatamani mchezaji huyo apone mapema.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Pole Sana kijana

    Jibu

    pole yake

    Jibu

    Dah

    Jibu

Acha ujumbe