Enzo Fernandez Azungumzia Uvumi kuhitajika Liverpool

Enzo Fernandez avunja ukimya kuhusu mustakabali wake Benfica huku kukiwa na taarifa za kuhitajika Liverpool kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari.

 

Fernandez

Kumekuwa na taarifa kwamba Liverpool wamekuwa wakihusishwa kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa Benfica, ambaye alionyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Fernandez aliisaidia Argentina kushinda mashindano hayo kwa mara ya tatu katika historia ya nchi hiyo.

Fernandez alihusishwa na kuhamia Liverpool kabla ya Kombe la Dunia, Baada ya kiwango chake cha kuvutia nchini Qatar, imesababisha uvumi mkali kuhusu mustakabali wake.

Inasemekana kuwa mchezaji huyo ana kipengele cha kutolewa chenye thamani ya €120million (£106m) katika mkataba wake na Benfica. Ripoti pia zimeeleza kuwa Manchester United na Newcastle pia wana nia ya kumsajili kiungo huyo.

 

Fernandez

Fernandez amerejea Argentina pamoja na wachezaji wenzake wakati anasherehekea ushindi wa nchi yake katika Kombe la Dunia. Na imeripotiwa kuwa mchezaji huyo alihutubia umati wa mashabiki katika mji wa San Martin katika nchi yake.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, Fernandez anaonekana alipuuza uvumi unaomhusisha na kuhamia Liverpool.

“Sijui chochote kuhusu hilo,” Fernandez alisema, kupitia Ge Globo.com. “Ni juu ya wakala wangu, sitaki kujihusisha.

“Ninaelekeza nguvu zangu kwa Benfica, ndani ya siku chache tuna mchezo muhimu. Ninawahi ndege usiku kucheza mchezo siku ya Ijumaa.”

Liverpool wako tayari wamekubali dili la kumsaini Cody Gakpo, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi akitarajiwa kufika Merseyside kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

 

Fernandez


Bashiri na kitochi au bila bando mechi hii, Bonyeza hapa kutazama ODDS kubwa na bomba kupitia machaguo spesho ya meridianbet ili kuingia mchezoni. Pia ukibashiri na kitochi kwa dau la TZS 1,000/= Unaweza kuibuka mshindi wa MBUZI WA KITOWEO CHA SIKUKUU, kila wiki Ijumaa.

Acha ujumbe