Grealish Aonyesha Kujuta Juu ya Maoni yake Kuhusu Almiron

Jack Grealish ameonyesha majuto kwa maoni yake ya kudhalilisha kuhusu mchezaji mwenzake wa Newcastle United Miguel Almiron, akikiri hilo lilikuwa jambo moja ambalo anajutia.

 

Grealish Aonyesha Kujuta Juu ya Maoni yake Kuhusu Almiron

Winga huyo wa Manchester City alimlenga mwenzake wa Newcastle United baada ya ushindi wa Ligi Kuu wa Manchester City mwanzoni mwaka huu, huku kukiwa na klip inayotembea mtandanoni Grealish akisema kuwa kufanyiwa mabadiliko Riyad Mahrez dhidi ya Aston Villa siku ya mwisho ni kwasababu alicheza kama Almiron.

Akisema kuwa uchezaji huo ulikuwa usiofaa akimlenga mchezaji huyo wa Kimataifa wa Paraguay, lakini hata hivyo Almiron alifurahi kuimarika kwa kiwango chake msimu huu na ameshinda tuzo ya mchezaji bora ya mwezi wa Ligi kuu na bao bora la mwezi Oktoba baada ya kufunga mara sita katika michezo sita.

Grealish Aonyesha Kujuta Juu ya Maoni yake Kuhusu Almiron

Alipokuwa akirejelea tukio hilo baya, Grealish aliweka wazi heshima yake kwa mchezaji huyo wa zamani wa Atlanta United, ambaye anafurahi kumwona akifanya vyema katika ligi kuu ya Uingereza.

Grealish Aonyesha Kujuta Juu ya Maoni yake Kuhusu Almiron

Grealish alisema kuwa; “Kwa kweli sijaulizwa kuhusu hilo na wacha nishughulikie” mchezaji huyo Kimataifa wa Uingereza aliambia The Independent. “Ilikuwa siku moja baada ya msimu kumalizika, na ni wazi nilikuwa na vinywaji vichache.”

Anasema kuwa mara baada ya hapo hakugundua kwa sababu walikuwa wanasherehekea, na hakuwa kwenye simu yake kwenye mitandao ya kijamii kwani anakumbuka alikuwa Ibiza na ni wazi imetoka. Hilo ni jambo moja ambalo najuta.

Grealish yuko kibaruani na Uingereza kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar, akionekana kama mchezaji wa akiba katika mechi zote tatu hadi sasa, huku akifunga bao la mwisho katika ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Iran.

Grealish Aonyesha Kujuta Juu ya Maoni yake Kuhusu Almiron

Winga huyo atatarajia kucheza tena Jumapili, wakati vijana wa Gareth Southgate watakapomenyana na Senegal kwenye Uwanja wa Al Bayt kuwania kufuzu kwa robo fainali.

Acha ujumbe