Kocha mkuu mpya wa Wolves Julen Lopetegui  apata wasiwasi baada ya Raul Jimenez kuteuliwa katika kikosi cha Mexico kitakachoshiriki Kombe la Dunia licha ya kutocheza tangu Agosti.

 

Lopetegui Ahofia Jiminez Kujumuishwa Kwenye Kombe la Dunia

Kocha wa zamani wa Sevilla na Real Madrid Lopetegui alianza rasmi kuinoa Wolves Jumatatu lakini atalazimika kusubiri hadi baada ya mapumziko ya Kombe la Dunia kwa mchezo wake wa kwanza.

Jimenez amecheza mechi tatu pekee za Ligi kuu ya Uingereza msimu huu, jumla ya dakika 211, baada ya kusumbuliwa na jeraha la paja lakini bado amejumuishwa kwenye orodha ya wachezaji 26 wa Mexico watakaosafiri kwenda Qatar.

Huku Wolves wakiwa wamesalia na pointi nne za usalama wakiwa mkiani mwa Ligi kuu ya Uingereza, huku  Lopetegui akisema kuwa ana  wasiwasi mkubwa baada ya mchezaji huyo kuitwa kwenye kushiriki michuano ya Kombe la Dunia.

Lopetegui Ahofia Jiminez Kujumuishwa Kwenye Kombe la Dunia

Kocha huyo alisema kuwa; “Jambo muhimu zaidi sio Kombe la Dunia, ni Wolves na amezungumza na Raul na pia nina wasiwasi naye kwasababu hachezi dakika moja na timu yake.”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwepo Molineux katika mechi waliyopokea kichapo cha 2-0 dhidi ya Arsenal Jumamosi kabla ya kutangazwa katika kikosi cha Mexico ambacho kinajumuisha Hirving Lozano wa Napoli na mlinzi wa Ajax Edson Alvarez.

Lakini hakukuwa na nafasi kwa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez, ambaye alifunga mabao 18 katika mechi 34 za MLS akiwa na Los Angeles Galaxy mnamo 2022.

Lopetegui Ahofia Jiminez Kujumuishwa Kwenye Kombe la Dunia

Vijana wa Martino wanaanza kampeni yao ya Kombe la Dunia dhidi ya Poland mnamo Novemba 22 kabla ya kumenyana na Argentina na Saudi Arabia katika Kundi C.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa