Mchezaji wa Everton Moise Kean anakabiliwa na faini ya paundi 100,000 pamoja na hasira ya meneja Carlo Ancelotti baada ya kukiuka sheria za kujilinda na Uviko-19 kwa kufanya Tafrija kwenye nyumba yake.

Mshambuliaji huyo wa Italia alituma picha za tukio hilo katika nyumba yake iliyopo Cheshire, ukiwa na wanawake kadhaa wanaoaminika kuwa wanamitindo, kwenye mtandao wa kijamii wa Snapchat.
Everton, ambao wamekuwa makini katika kuwasaidia mashabiki katika jumuiya yao kukabiliana na matatizo ya kujitenga, walikasirika baada ya kujifunza kuhusu tabia ya Kean.
Maafisa wa ngazi za juu wa Goodison wanaeleweka kusikitishwa kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 alionyesha utovu wa nidhamu na kujitambua na wamemwacha bila shaka kwamba vitendo vyake havikubaliki.
Bosi wa Everton Ancelotti amesikitishwa sana kwamba Kean amejiangusha na anaweza kutarajia kuwa kupigwa faini ya zaidi ya £100,000, ambayo ni sawa na mshahara wa wiki mbili. Wakati Ligi nyingi zimesimama kupisha michuano ya kombe la dunia. Meridianbet wanakupa machaguo spesho ya kubeti na kitochi, ODDS kubwa na bomba, cha kufanya ni kubeti bila bando mechi nyingi. Beti hapa.

Everton hawakupoteza muda kutoa taarifa. Ilisomeka hivi: “Klabu ya Soka ya Everton ilishtuka kusikia tukio ambalo mchezaji wa kikosi cha kwanza alipuuza mwongozo wa Serikali na sera ya klabu kuhusiana na janga laUviko-19.
“Klabu imeeleza vikali kusikitishwa kwake na mchezaji huyo na kuweka wazi vitendo hivyo havikubaliki kabisa.
“Everton imesisitiza mara kwa mara umuhimu wa kufuata miongozo yote ya Serikali, ikiwa ni pamoja na sheria na ushauri wa ndani na nje ya nyumba, kupitia mfululizo wa mawasiliano rasmi kwa wafanyakazi wote, ikiwa ni pamoja na wachezaji.
“Watu wa ajabu katika NHS wanastahili heshima kubwa kwa bidii na kujitolea kwao. Njia bora zaidi ya kuwaonyesha heshima ni kufanya kila tuwezalo ili kuwalinda.”
Wakala wa Kean, Mino Raiola hakupatikana kuzungumzia suala hilo, lakini vyanzo vya karibu vilithibitisha kwamba Kean aliomba radhi kwa klabu kwa aibu aliyoisababisha na kuapa kuwa haitajirudia.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.


