Jadon Sancho ameoneka akifanya mazoezi nje ya Manchester United na hatarejea hadi atakapokuwa tayari kimwili na kiakili kuichezea klabu hiyo tena.

 

sancho

Sancho amekuwa akifanya kazi Uholanzi na makocha wanaoaminiwa na meneja wake Erik ten Hag, Sancho hajaichezea Manchester United tangu Oktoba 22 kutokana na ugonjwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikosa kambi ya mazoezi ya klabu hiyo nchini Hispania wiki iliyopita baada ya kuachwa nje ya kikosi cha England kilichoshiriki Kombe la Dunia.

Sancho, ambaye alijiunga na United miezi 18 iliyopita kwa paundi milioni 73 kutoka Borussia Dortmund, alizima akaunti zake za mitandao ya kijamii mwezi uliopita ili kuwa karibu na familia yake na nusu ya pili ya msimu, kulingana na vyanzo.

 

sancho

Ten Hag amezungumza na fowadi huyo kuhusu hali yake mara kadhaa na hakutaka kuweka muda kuhusu lini Sancho atarejea mazoezini.

“Sidhani kama atarejea wiki hii, hapana,” alisema Ten Hag.

“Tunataka kumrejesha haraka iwezekanavyo, lakini siwezi kutoa ubashiri wa lini hiyo itakuwa, wakati mwingine kuna hali na usawa na mhemko. Tumepata kushuka kwa kiwango cha ubora na wakati mwingine hujui ni kwa nini au ni nini kinachosababisha.

 

sancho

“Hicho ndicho tunachofanya sasa kujaribu kumrudisha huko. Ni mchanganyiko wa kimwili na kiakili.”

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa