Beki wa kati wa Liverpool Virgil van Dijk amesema Liverpool “haijawahi kutilia shaka” ubora wa Darwin Nunez kufuatia kuimarika kwa mshambuliaji huyo hivi karibuni baada ya kuwa na mashaka mengi juu yake.

 

Van Dijk: "Liverpool Haijawahi Kutilia Shaka Ubora wa Nunez"

Nunez alistahimili mwanzo mbaya wa maisha Anfield kufuatia uhamisho wake wa pesa nyingi kutoka Benfica, akipokea kadi nyekundu dhidi ya Crystal Palace katika mechi yake ya tatu pekee chini ya Jurgen Klopp.

Hata hivyo, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uruguay anaanza kupiga hatua katika soka la Uingereza ambapo ametupia mabao mawili katika ushindi wa 3-1 Jumamosi dhidi ya Southampton na kufikisha jumla ya mabao yake kwa msimu huu hadi tisa.

Huku mchezaji mwenzake Van Dijk akisema kuwa; “Hatukuwahi kutilia shaka ubora wake lakini ni wazi, unapokuwa na bei kama hiyo na malengo hayaendi kama unavyotaka, ni vizuri ameonyesha tabia nzuri na nadhani amefanya vizuri sana”

Van Dijk: "Liverpool Haijawahi Kutilia Shaka Ubora wa Nunez"

Van Dijk aliongezea kwa kusema kuwa Nunez ana sifa zote kwa mshambuliaji wa kisasa na kuna sababu tulimnunua na anakomaa, amekuwa mvumilivu, ameweka chini na kucheza na hiyo ni sifa kwake, pia ana matumaini anaweza kuendelea kufunga na kuwa muhimu kwa kikundi.

Inachukua muda. Ni timu mpya, mazingira mapya, nchi mpya, lugha mpya, hivyo ni kawaida kabisa kwake kuchukua muda kidogo zaidi kutulia lakini hakuna shaka sifa zipo, na malengo yatafuata.

Van Dijk: "Liverpool Haijawahi Kutilia Shaka Ubora wa Nunez"

Van Dijk pia alimmwagia sifa mlinda mlango Alisson, ambaye aliokoa michomo iliyokuwa inalenga lango lao  walipokuwa wakicheza dhidi ya Southampton wakati wa ushindi wa Anfield.

Nahodha huyo wa Uholanzi pia aliangazia tabia ya Roberto Firmino, huku mshambuliaji huyo akifungua ukurasa wa mabao dhidi ya Saints baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Van Dijk: "Liverpool Haijawahi Kutilia Shaka Ubora wa Nunez"

Beki huyo alisema kuwa; Brazil ni timu nzuri sana, wana makipa wao wawili bora kwenye kikosi chao na kwa maoni yangu, kipa bora duniani ni Alisson, na ninadhani Bobby anafaa kuwa ndani, lakini yeye ni nani kusema hivyo?


beti na kitochi

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa