Imeripotiwa kwamba mshambuliaji wa klabu ya Burnley Wout Weghorst anayekipiga kwa mkopo kwenye klbau ya Besiktas nchini Uturuki, anataka kujiunga Manchester United kwa mkopo kupitia dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. Meridianbet wana Maduka ya Kubashiri kote nchini.

 

Weghorst

Mholanzi huyo hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford huku United wakipania kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

Kocha wa timu hiyo Erik ten Hag huenda akafanya kazi pamoja na Mholanzi mwenzake, huku Weghorst sasa akitaka kuhama.

Mshambuliaji huyo amekuwa kwa mkopo Besiktas kutoka Burnley kwa kipindi cha kwanza cha msimu wa 2022/23.

Hata hivyo, timu hiyo ya Uturuki imekubali kusitisha mkopo huo mapema ili kuruhusu uhamisho wa kwenda United kufanyika.

Ten Hag anaamini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ataweza kuongeza mwelekeo tofauti kwenye mashambulizi ya Red Devils.

Weghorst anaonekana kucheza mchezo wake wa mwisho kwa Besiktas, akifunga bao la ushindi katika ushindi wa 2-1 wa ligi dhidi ya Kasimpasa. Unaweza kubashiri Mubashara na Meridianbet Bonyeza hapa.

Sasa hivi karibuni anaweza kurejea Ligi ya Uingereza, baada ya kucheza ligi kuu ya Uingereza katika klabu ya Burnley msimu uliopita.

Fowadi huyo alikuwa mmoja wa mashujaa wa Uholanzi wakati wa Kombe la Dunia huko Qatar.

Aliingia akitokea benchi na kufunga bao muhimu la kusawazisha katika dakika ya 11 ya dakika za lala salama dhidi ya Argentina. Pata Oddskubwa za Soka hapa.

 

Weghorst

Ingawa Waholanzi walishindwa hivi karibuni na mabingwa wa Kombe la Dunia, ilikuwa moja ya matukio ya kushangaza zaidi nchini Qatar.

Weghorst tayari ana mabao tisa ya klabu hadi sasa msimu huu, idadi ambayo inaweza kuongezwa kwenye EPL miezi ijayo.

Anaweza kujiunga na kikosi cha United ambacho kinajiamini, huku Mashetani Wekundu wakiwa nafasi ya nne kwenye jedwali baada ya mechi 17.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa