Liverpool wanaweza kupiga hatua ya karibu sana kubeba taji lao la kwanza la ligi baada ya miaka 30 wakati watakapokabiliana na maasimu wao wakubwa Everton Jumapili hii katika dimba la Goodison Park. ‘The Reds’ wamekuwa kwenye kiwango bora sana kwenye Ligi msimu huu na kwa sasa wanaongoza kwa tofauti ya alama 22 kileleni mwa msimamo wa EPL huku zikiwa zimebaki mechi tisa.

, Super Sunday, Mshike Mshike wa EPL Leo jumapili 21-06-2020, Meridianbet

Kikosi cha Jurgen Klopp sasa kinahitaji kushinda michezo miwili tu kutwaa taji la Ligi na hakuna kitu inaweza kuwa furaha kwa mashabiki wa Liverpool kama kuchukua alama tatu kueleke ubingwa kutoka kwa wapinzani wao Everton.

Vijana wa Carlo Ancelotti bado wana nafasi ndogo ya kufuzu Ligi ya Europa kwa msimu ujao. Wako katika nafasi ya 12 alama saba tu nyuma ya Sheffield United iliyopo katika nafasi ya sita.

Everton Kama wataweza kufuzu mashindano ya Europa utakuwa msimu mzuri kwao kutokana na ambavyo walianza vibaya sana na hata kumfukuza kocha Marco Silva mapema msimu huu.

, Super Sunday, Mshike Mshike wa EPL Leo jumapili 21-06-2020, Meridianbet

Je! Everton Wanaweza kupata matokeo leo na kutengeneza mazingira ya kufuzu Europa? Au Liverpool watachukua alama tatu kuusogelea ubingwa wa Ligi?
Michezo mingine Leo EPL:
Newcastle v Sheff Utd (16:00)
Aston Villa v Chelsea (18:15)

51 MAONI

  1. Hawa Everton walimsema sana kocha wao Marco hadi kumtimua sasa leo wataweza kudhibitisha kuwa kocha alikuwa anawapoteza au walikuwa wanapotezana leo siyakukosa hii mechi

  2. Mechi ya Everton vs Liverpool haijawahi kuwa nyepesi hata kidogo. Everton inaweza ishangaza dunia kwa kushinda mechi ya leo#meridianbettz

  3. Leo mechi zote kali si epl wala la liga ila hii ya Liverpool kazi ipo leo maana huawaga si nyepesi kupata ushindi inawezekana everton wakawacheleweshea ubingwa Liverpool leo

  4. Goodeson park uwanja wa everton kitachimbika pale ,vinara hao wa uingereza wakikipiga na waasimu wao everton.huku liverpool wanahitaji arama3 ili kuendelea kujikita kileleni

  5. kiukweli yani hapo kwa everton kumfunga livepool daah ni ndoto coz live yupo kwe form yan inabidi afanye kaz kweli

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa