EURO 2020: Mashabiki Kutoka UK Kutoingia Uwanjani

Ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya michezo ya robo ya Euro 2020 kuendelea tena katika viwanja vinne tofauti, taariafa rasmi kutoka Italia ambapo England watacheza dhidi ya Ukraine zinasema kuwa mashabiki kutoka Uingereza hawatoruhusiwa kuingia uwanjani.

Taarifa hiyo kutoka Rome inasema kuwa hata kama mashabiki wa Uingereza au mtu yeyote atakayetoka Uingereza hatoruhusiwa kuingia kushuhudia mechi hiyo endapo hatokuwa katimiza siku tano akiwa kwenye eneo la kujitenga!

Uingereza ilifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya Euro 2020 baada ya kuvunja historia iliyo dumu kwa miongo kadhaa ya kufungwa na Ujerumani baada ya kuwachapa bao 2-0.

Licha ya michuano hii ya Euro 2020 kushuhudiwa na watu wengi sana, bado taratibu sahihi za kuzuia ueneaji wa ugonjwa wa Corona unazingatiwa.

Juzi iliripotiwa kuwa takribani watu 2000 kutoka Scotland ambao walisafiri kwenda Uingereza walirejea na kugundulika kuwa wamepata Corona licha ya watu hao kuwa na kinga au kuonesha hawakuwa na Corona kabla ya mchezo.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe