Huu ni msimu ambao klabu ya Arsenal inaendelea kutaabika kunako msimamo wa EPL (nafasi ya 9 kwa sasa). Kocha Mikel Arteta, analivutia kasi taji la Europa msimu huu.

Arsenal watakuwa uwanjani leo usiku katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Villareal. Arteta ataiongoza Arsenal ikiwa na matokeo ya kupoteza kwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza.

Licha ya kupotezea mchezo wa kwanza, Arsenal waliibuka kidedea wikiendi hii kwenye EPL kwa kuwafunga Newcastle United. Hii inawapa motisha zaidi vijana wa Mikel kuelekea mchezo ambao wanahitaji ushindi kwa namna yeyote.

Endapo Arsenal wataweza kupindua matokeo, wananafasi kubwa ya kuchuana na Man United kwenye mchezo wa fainali ya Europa. Hii itakuwa ni mara ya pili wanafuzu hatua ya fainali dhidi ya timu ya EPL kama ilivyokuwa mwaka 2019 ambapo walifungwa na Chelsea (4-0).

“Ni jambo kubwa. Sio kwangu, bali kwa kila kitu kilichotokea kwenye klabu kwa miaka miwili na miezi iliyopita. Nadhani itakuwa ni kitu cha muhimu sana kama tutaweza kuingia hatua ya fainali na kufanikiwa kutwaa ubingwa.” amesema Mikel Arteta.

Swali ni je, Arsenal wataweza kupindua matokeo leo usiku? Ikitokea Arsenal wamefanikiwa kubeba ubingwa wa Europa, watakuwa wamefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao bila kuangalia watamaliza msimu wa EPL wakiwa kwenye nafasi gani msimu huu.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Arteta, Arteta Analivutia Kasi Taji la Europa., Meridianbet

SOMA ZAIDI

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa