Katika kila kitu, kuna pande mbili. Kwenye soka ni zaidi, matokeo yapo ya aina 3. Imekuwa hivyo kwenye Ligi ya Europa msimu huu.
Katika mzunguko wa pili wa michezo ya nusu fainali. Arsenal waliwaalika Villareal huku Man United wakiwafuata AS Roma kule nchini Italia.
Arsenal walikuwa wanahitaji ushindi wa 1-0 pekee ili wafuzu hatua ya fainali huku United wakiwafuata Roma huku wanafaida ya magoli 4 mkononi. Mambo yalikuwa tofauti sana.
Matokeo ya sare (0-0) kwa Arsenal, yamewakatisha kwenye safari yao ya kushiriki mashindano ya Ulaya kwa misimu 25 mfululizo. Licha ya United kufungwa 3-2, wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ikiwa ni fainali yao ya 8 kwenye mashindano ya Ulaya.

Kupoteza nafasi ya kucheza fainali ya Europa, kunawaeka Arsenal kwenye nafasi ya kutoshiriki mashindano yeyote ya ulaya msimu ujao endapo hawatofanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya 6 za juu kwenye msimamo wa EPL kwa michezo iliyosalia msimu huu.

Kwa United, kutinga hatua ya fainali ya Europa ndio nafasi pekee ya kubeba taji msimu huu. Ole Gunnar Solskjaer anakibarua cha ziada kufuatia kuwa na jumla ya michezo 6 ndani ya muda mfupi. Alipoteza michezo 5 ya nusu fainali tangu amekabidhiwa timu. Je, fainali yake ya kwanza ataitoa United kimasomaso?
Hakika mwenzako akilia, kuna mwingine anacheka!
TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO
Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!
Ni kujipanga upya tu
Wajipange upya
Wajipange vizuri
Waongeze juhudi
Wajipange vizuri
Wasikate tamaa
Waongeze juudi
Duh balaa
Noma sana