Manchester United dhidi ya Real Betis 16 Bora Europa League

Klabu ya Manchester United imerudishwa tena nchini Hispania ni baada ya kupangwa na klabu ya Real Betis kwenye michuano ya Uefa Europa league hatua ya 16 bora baada ya droo kuchezeshwa mchana wa leo.

Klabu ya Manchester United baada ya kuitupa nje klabu ya Barcelona hapo jana kwenye hatua ya 32 bora shirikisho la soka barani ulaya baada ya kuchezesha droo wameirudisha klabu hiyo nchini Hispania kwa mara nyingine baada ya kupangwa na klabu ya Real Betis chini ya kocha Manuel Pellegrini.manchester unitedMashetani wekundu mpaka sasa kwenye michuano ya Europa league wameshakutana na vilabu viwili kutoka nchini Hispania, Kwani kwenye hatua ya makundi walipangwa na klabu ya Real Sociedad na katika hatua ya 32 bora wakipangwa na klabu ya Fc Barcelona na kufanikiwa kuitupa njeya michuano hiyo.

Klabu ya Manchester United imekua kwenye kiwango bora msimu huu na hiyo inaendelea kujidhihirsha kila siku, Kwani mpaka sasa ni klabu pekee kutoka ndani ya ligi kuu ya Uingereza inashiriki michuano yote minne mpaka sasa jambo ikiwa ni mafanikio kwa klabu hiyo ukilinganisha na misimu kadhaa nyuma.manchester unitedManchester United wanatarajiwa kucheza dhidi ya klabu ya Newcastle wikiendi hii katika mchezo wa fainali ya kombe la Carabao unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Wembley siku ya jumapili, Mchezo huu unaweza kuipatia Man United taji la kwanza baada ya kupita takribani miaka sita tangu kubeba taji lao la mwisho.

Acha ujumbe