Kocha wa Tottenham – Jose Mourinho ameibuka na kusema hadharani kuwa anamashaka na mitazamo ya baadhi ya wachezaji wake.

Habari hii imetokea katika mchezo wa Ligi ya Europa ambapo Spurs walijikuta wakilazimishwa kutoka sare na LASK kwa matokeo ya 3-3.

Mchezo ambao baadhi ya wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi kwenye kikosi cha Mourinho walipewa nafasi lakini walishindwa kuonesha cheche zao kama ambavyo wengi walidhani itatokea.

Mourinho
Gareth Bale akipachika goli kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha kwanza.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Jose amenukuliwa akisema “Nadhani ni suala la mtazamo, nimewahi kupitia hilo hata wakati nilipokuwa Manchester United.

“Nilikuwa na hali kama hii – tulifungwa michezo miwili ya ugenini katika hatua ya makundi. Tunapoingia hatua ya mtoano, tunakutana na wapinzani bora zaidi, michezo inakuwa ni migumu na mechi zinakuwa tofauti.”

Baada ya kuulizwa kama amejifunza kitu chochote, Mourinho alisema “Hakuna jipya, uhalisia ni kwamba wachezaji wengi hawashawishiki na hatua ya makundi kwenye Ligi ya Europa. Ninalijua hilo.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Mourinho, Mourinho Anamashaka na Mitazamo ya Wachezaji, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa