Moyes Amsifu Paqueta Huku Wakiendeleza "Unbeaten" Yao

David Moyes alimpigia saluti Lucas Paqueta baada ya ushindi wa 2-1 wa Ligi ya Europa dhidi ya Freiburg na kuihakikishia West Ham kuweka historia yao ya kutopoteza mechi 17 barani Ulaya.

 

Moyes Amsifu Paqueta Huku Wakiendeleza "Unbeaten" Yao

Mshambuliaji huyo wa Brazil aliwaweka Wagonga nyundo mbele baada ya dakika tisa pekee kwa mpira wa kichwa kutoka kwa krosi ya Jarrod Bowen na Nayef Aguerd akahitimisha ushindi huo kwa kichwa kingine katika kipindi cha pili.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Ushindi huo unawaacha Wagonga Nyundo hao wakiwa kileleni mwa Kundi A baada ya kuanza vyema kampeni zao za Ligi ya Europa na kuwafanya kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kucheza mechi 17 bila kushindwa katika soka la Ulaya.

Moyes Amsifu Paqueta Huku Wakiendeleza "Unbeaten" Yao

Moyes alisema: “Lilikuwa ni bao la kizamani, chini ya upande na krosi nzuri, na kisha kupiga kichwa kizuri kama mshambuliaji wa kati wa mtindo wa zamani. Nilifurahia sana kulitazama. Jarrod alicheza vizuri lakini Lucas alikuwa mzuri. Ananitia wazimu wakati mwingine lakini kila mtu aliyemtazama angesema mchezaji huyu ana kipaji cha ajabu.”

Moyes aliongeza kuwa mchezaji huyo ni muhimu sana kwao na wanafurahi sana kwasasa ana uwezo mkubwa wa kuchukua mpira chini ya shinikizo lakini pia kuna nyakati ambapo yeye husema atafanya nini.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Moyes Amsifu Paqueta Huku Wakiendeleza "Unbeaten" Yao

Freiburg walisawazisha baada ya muda wa mapumziko kupitia kwa Roland Sallai, lakini mpira wa kichwa wa Aguerd kutoka kwa mpira wa kona wa James Ward-Prowse ukawarudisha nyumbani.

Katika rekodi hiyo, Moyes aliongeza: “Ni mafanikio ya ajabu, nimesema kwa vijana tunatakiwa kuyaendeleza. Kushinda mchezo wa leo usiku ilikuwa muhimu zaidi.”

Acha ujumbe