Kuelekea mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Europa, klabu ya AS Roma imatangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaochuana na Manchester United leo usiku.

Roma wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na deni la magoli 4 baada ya kufungwa 6-2 kwenye mchezo wa kwanza. Miamba hii ya soka la Italia, inahistoria ya kupindua matokeo na kufuzu kwenye mashindano mbalimbali.

Pau Lopez, Leonardo Spinazzola, Jordan Veretout, Amadou Diawara, Gonzalo Villar na Carles Perez watakosekana kwenye mchezo huu. Lorenzo Pellegrini, Pedro Rodriguez na Gianluca Mancini wamerejea tena kikosi na wapo tayari kupambana na Man United.

Kikosi kitachopigania nafasi ya AS Roma dhidi ya Manchester United:

Magolikipa: Simone Farelli, Daniel Fuzato, Antonio Mirante
Walinzi: Rick Karsdorp, Roger Ibanez, Chris Smalling, Davide Santon, Gianluca Mancini, Marash Kumbulla, Bruno Peres
Viungo: Bryan Cristante, Lorenzo Pellegrini, Edoardo Bove, Riccardo Ciervo, Ebrima Darboe, Nicola Zalewski, Henrikh Mkhitaryan
Washambuliaji: Edin Dzeko, Pedro Rodriguez, Borja Mayoral


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Roma, Roma Yatangaza Wapiganaji 20 vs United., Meridianbet

SOMA ZAIDI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa