Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo amerejea kwwenye kikosi na kufunga bao lake hapo jana kwenye ushindi wa 3-0 kwenye michuano ya Europa walipokuwa wakicheza dhidi ya Sheriff na kuiwezesha timu yake kuwa na matumaini ya kwenda hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa.
Mabao mawili ya vichwa kutoka kwa Diego Dalot na Marcus Rashford yaliiweka United mbele kabla ya Ronaldo kumalizia pointi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika na hivyo kufanikiwa kumaliza katika nafasi mbili za juu katika Kundi E.
Kikosi cha Erik ten Hag sasa lazima kiwafunge vinara wa kundi hilo, Real Sociedad katika mechi ya mwisho wiki ijayo ili kiweze kuongoza kundi hilo kuepuka kupangiwa timu ngumu katika raundi ya mtoano.
Wakiwa wamejihakikishia kumaliza katika nafasi mbili za juu katika Kundi E, United sasa watajikita zaidi katika kufuzu kwa raundi ya mchujo ya Ligi ya Europa, huku Juventus na Barcelona wakiwa tayari ni miongoni mwa timu zilizo katika nafasi ya tatu kushuka kutoka Ligi ya Mabingwa.
Kwa upande wa Sheriff, ambaye amekuwa na mwenendo mbaya katika michuano hiyo anaonekana hawezi tena kuendelea na michuano hiyo hivyo atashuka kwenda kucheza Konferensi. Na sasa wamepoteza mechi nne mfululizo katika mashindano makubwa ya Ulaya kwa mara ya kwanza.
Ronaldo na wenzake watarejea uwanjani Jumapili kabla ya kukamilisha kampeni za hatua ya makundi wiki ijayo. United inawakaribisha West Ham katika Ligi ya Uingereza huku vonara wa Superliga Sheriff wakiwakaribisha Dacia-Buiucani.