Ten Hag Apagawa Baada ya Kushindwa Kuongoza Kundi

Kocha mkuu wa Manchester United Erik ten Hag amekiri kuvunjika moyo baada ya timu yake kushindwa kuongoza kundi lao la Ligi ya Europa licha ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Sociedad hapo jana.

 

Ten Hag Apagawa Baada ya Kushindwa Kuongoza Kundi

Kama United ingepata ushindi wa mabao mawili au zaidi ungewafanya kusonga mbele kama vinara wa Kundi E kwasababu ya rekodi ya juu zaidi ya uso kwa uso dhidi ya Real ya Uhispania.

Bao la United lilifungwa na  Alejandro Garnacho dakika ya 17 na kuipa  matumaini timu yao lakini hilo likawa ndio shuti lao pekee lililolenga lango wakati wa mchezo ambao ulikuwa wa kiushindani kwelikweli katika uwanja wa Reale Arena.

Ten Hag a,mesema kuwa “Kwa kweli, tumesikitishwa hatukufunga mabao mawili kwa sababu ndicho tulichohitaji. Tunataka kila mara kuwa nambari 1 na wakati hatupo, tunakatishwa tamaa.”

Ten Hag Apagawa Baada ya Kushindwa Kuongoza Kundi

Ten Hag alionyesha matokeo chanya kwenye mchezo huo, huku akifurahia Garnacho kupata bao hilo akiwa na umri mdogo wa 18 na kuwa mfungaji bora wa United ambaye si Muingereza katika mashindano makubwa ya Ulaya, akichukua rekodi hiyo kutoka kwa gwiji wa klabu George Best.

Kocha huyo alisema kuwa wameshinda na wamefurahishwa na jambo hilo na mambo mengine kama uchezaji wa Alejandro Garnacho huku akigusia wachezaji waliokuwa nje kama Antony, Jadon Sancho hakupatikana na anatumaini kwamba anaweza kuendeleza mchakato huo.

Ten Hag Apagawa Baada ya Kushindwa Kuongoza Kundi

Acha ujumbe