Everton: Vigogo Wamegawanyika Kwa Rooney.

Bado ni hali ya sintofahamu kule Everton linapokuja suala la kocha mpya baada ya Rafa Benitez. Bodi ya wakurugenzi imegawanyika kwa Wayne Rooney.

Wakati mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright akimpigia pande Rooney kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, baadhi ya viongozi wa bodi (pamoja na mmiliki – Farhad Morshiri), hawamuoni Rooney kama mtu sahihi.

Kwa Morshiri kikwazo kikubwa ni uzoefu wa Rooney kwenye nafasi ya ukocha. Kwa sasa, Wayne anapambana na Derby County ambayo ipo kwenye majanga ndani na nje ya uwanja. Uzoefu wake wa ukocha, haumpi nafasi kubwa ya kukabidhiwa timu kama Everton kwa namna Morshiri na baadhi ya viongozi wanavyomtizama.

Japokuwa Rooney ni miongoni mwa wachezaji wazawa na wenye heshima kubwa Goodison Park, uwezo wake kama kocha, haumbebi sana kwenye nafasi hiyo. Kwa hali ilivyo, Duncan Ferguson ataiongoza klabu hiyo kwa muda wakati mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe