Burudani ya soka imeendelea tena viwanjani wiki hii. Middlesbrough au ukipenda waite ‘Boro’ wamendelea kuchana mikeka.

Ni wale wale vijana wa Chris Wilder ambao walizamisha jahazi la Manchester United kule Old Trafford, ndio wamepeleka kilio kingine kwa Antonio Conte kunako FA Cup.

Boro waliwalaza na viatu Man United kwenye mzunguko wa 4 licha ya kwamba, ni timu ambayo inapambania kutafuta nafasi za kupanda ligi kuu (EPL) msimu ujao. United walipoteza mchezo wakiwa Old Trafford na Middlesbrough wakasonga mbele.

Unaambiwa hivi, usimdharau usiyemjua. Lakini pia, zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Huyu ni Chris Wilder, timu zilizokutana naye wakati akiiongoza Sheffield United kwenye EPl zinamjua vizuri. Mfumo wake wa 3-5-2 ni silaha ya maangamizi kwa wapinzani. Haitaji wachezaji wenye majina makubwa kwenye timu yake lakini, hao hao tunaowaita wachezaji wa kawaida ndio wanaompatia matokeo.

Boro, Boro Imeendelea Ilipoishia Old Trafford., Meridianbet

Alianza kuzamisha jahazi la United kwenye kinyang’anyiro cha kuwania taji msimu huu, na sasa amemalizia safari ya Conte kwenye mashindano tofauti na EPL. Sio Harry Kane, wala sio Son aliyeweza kuwachachafya walinzi au golikipa wa Boro, lakini, mchezaji kinda ambaye aliingia uwanjani akitokea benchi (Josh Coburn) alitosha kuzamisha jahazi la Tottenham kwa kupachika goli dakika ya 107 na ushindi kwenda Middlesbrough.

Nani ni nani kunako hatua ya robo fainali ya FA Cup, tutatambuana vyema alhamisi hii wakati droo ya michezo ya hatua hiyo itakapochezeshwa.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa