Camera ilivuta kwa karibu zaidi majukwaa ya kaskazini wakati Frank Ribery akifanya yake, macho yakamuona mzee mmoja ameshika kichwa haamini kinachotokea. Sekunde chache tu zilizopita aliamini anasubiri dakika za nyongeza.

Nilimuona mtoto mmoja akimwaga machozi, hakuamini kama mechi imeamuliwa kikatili namna hii. Pengine aliwaaga rafiki zake kuwa anaenda Wembley kuitazama timu ya mtaani kwake ikibeba UEFA, lakini haikuwa hivo.

Frank Ribery
Frank Ribery
Nilimtupia macho Jurgen Klopp, macho yamemtoka ndani ya miwani yake kubwa kama dunia. Hajui hata atazame wapi. Ameshindwa kukaa, ameshindwa kusimama. Amebaki tu anacheka.

Ukuta wote wa Dortmund ulikuwa matatani tangu dakika ya kwanza, kila mpira aliogusa Frank Ribery ulikuwa ‘shubiri’ kwao, alishaanzisha safari ya bao la Mario Mandzukic kisha akaweka pasi ya kisigino kwa Arjen Robben, ni dakika ya 89 na Dortmund wanaletwa kati tena.

Matumaini yao ya kubeba UEFA yanafia hapo, kazi ngumu waliyofanya kuitoa Real Madrid ya Jose Mourinho nusu fainali ya UEFA imefia hapo. Shida yote hii imeletwa na mguu wa mfaransa mmoja aliyenusurika kifo utotoni.

Roben aliondoka Wembley akiwa mfalme lakini Ribery aliondoka akiwa shujaa. Lakini sawa, Ribery huyu aliikosa fainali ya 2010 kwasababu ya kadi. Ribery huyuhuyu alikuwepo waking’atwa na mbuzi 2012. Mara hii asingekubali tena.

Frank Ribery
Frank Ribery
Historia yangu ya Frank Henry Pierre Ribery inaanza asubuhi moja ya 1985 akiwa mtoto wa miaka miwili tu. Gari alilokuwa akiendesha baba yake lilipata ajali na kumsababishia majeraha makubwa. Angeweza hata kupoteza maisha.

Kwa Frank Ribery hii haikuwa ajali bali sehemu iliyotokea katika maisha yake ili imjenge na kumkomaza zaidi. Dhahabu hii lazima ipite kwenye moto ili ing’ae.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa