De Zerbi Anataka Kujiuzulu Olympique Marseille

Footmercato wanadai kuwa kocha wa Kiitaliano Roberto De Zerbi ameomba aachiwe mkataba wake na Olympique Marseille kufuatia kutolewa kwao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

De Zerbi Anataka Kujiuzulu Olympique Marseille

Timu hiyo ya Ligue 1 ilitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kupokea kipigo cha kushangaza cha mabao 3-0 dhidi ya Club Brugge katika raundi ya mwisho ya hatua ya ligi.

Kulikuwa na ripoti zilizosambaa mchana huu zikidai kuwa Olympique Marseille walikuwa wakitathmini nafasi yake na huenda walikuwa tayari kumaliza rasmi kipindi chake cha ukocha.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Habari kubwa iliyotolewa na Footmercato jioni ya leo ni dai kwamba De Zerbi mwenyewe aliomba klabu imruhusu aondoke, akihisi kuwa uhusiano wake na uongozi hauwezi kuendelea tena.

De Zerbi Anataka Kujiuzulu Olympique Marseille

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 ameiongoza Marseille kupata ushindi 17, sare mbili na vipigo 11 katika mashindano yote msimu huu.

Aliteuliwa msimu wa joto wa 2024, baada ya kufundisha klabu kadhaa zikiwemo Foggia, Palermo, Benevento, Sassuolo, Shakhtar Donetsk na Brighton & Hove Albion.

Endapo ataondoka Marseille, hilo linaweza kufungua mlango wa kurejea Serie A nchini Italia au Ligi Kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.