De Zerbi: Greenwood ni Mchezaji Mzuri Sana

Kocha mpya wa klabu ya Olympique Marseillle Roberto De Zerbi amemmwagia sifa winga wa Manchester United Mason Greenwood kua ni mchezaji bora na mwenye uwezo mkubwa.

Klabu ya Olympique Marseille inaelezwa kutuma ofa ya paundi milioni 27 kwa klabu ya Manchester United ili kuangalia uwezo wa kupata huduma ya winga huyo ambaye msimu uliopita amekipiga ndani ya klabuu ya Getafe ya nchini Hispania na ndio sababu ya kocha De Zerbi kuanza kumzungumzia winga huyo leo.de zerbiKocha De Zerbi leo wakati anazungumza na wanahabari aliweka wazi na kuzungumzia juu ya winga huyo kama atajinga nao“Hakika Mason ni mchezaji wa kiwango cha dunia.”

“Sijui historia yake. Haijalishi mchezaji ni nani… mara tu wanaposaini hapa, wanakuwa kama watoto wangu. Nawalinda daima.”

Klabu ya Olympique Marseille chini ya kocha Roberto De Zerbi imekua kwenye nafasi nzuri ya kumpata winga Mason Greenwood kwakua ndio klabu pekee ambayo imetuma ofa nzuri mpaka sasa, Huku klabu ya Man United ikiwa imeweka wazi iko tayari kumuuza kiungo huyo.

Acha ujumbe