Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Ousmane Dembele, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligue 1 kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuiongoza timu hiyo kukaribia kutwaa ubingwa wa 14 wa ligi kuu ya Ufaransa pamoja na kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Dembele mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na orodha ya wachezaji watano pekee waliowahi kushinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo, huku aliyekuwa wa mwisho kufanya hivyo akiwa Zlatan Ibrahimovic mwaka 2014. Msimu uliopita Dembele alimrithi Kylian Mbappe aliyekuwa ametwaa tuzo hiyo mara tano mfululizo kabla ya kuhamia Real Madrid.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza baada ya kutwaa tuzo hiyo, Dembele alisema mafanikio hayo yametokana na mchango wa wachezaji wenzake ndani ya kikosi cha PSG. “Ni tuzo binafsi, lakini tuzo zote binafsi nilizowahi kushinda ni kutokana na timu hii,” alisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Licha ya kusumbuliwa na majeraha msimu huu, Dembele ameendelea kuwa na mchango mkubwa kwa PSG. Ameanza katika michezo tisa pekee ya Ligue 1 na kucheza dakika 960, tofauti na msimu uliopita ambapo alianza mechi 20 na kucheza dakika 1,736.

Katika idadi hiyo ndogo ya mechi, Dembele amefunga mabao 10 na kutoa pasi sita za mabao, ingawa takwimu hizo zipo chini ya mabao 21 na pasi nane alizorekodi msimu uliopita. Ubora wake umeendelea kuonekana kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya PSG chini ya kocha Luis Enrique.
Kwa sasa PSG ipo hatua moja kutoka kutangazwa mabingwa wa Ligue 1 kwa mara ya tano mfululizo baada ya ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Brest mwishoni mwa wiki. Ushindi huo umeiweka PSG kileleni kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya Lens huku ikiwa na mchezo mmoja muhimu dhidi ya wapinzani hao Jumatano.


