Christophe Galtier ameshukuru kumrejesha Lionel Messi kama mshindi wa Kombe la Dunia akifunga katika ushindi wa 2-0 wa Paris Saint-Germain dhidi ya Angers hapo jana.
Nahodha huyo wa Argentina aliichezea klabu yake kwa mara ya kwanza tangu kunyanyua kombe mwezi uliopita, na PSG wakiwa mbele kwa bao 1-0 pekee dhidi ya klabu ya mkiani ya Ligue 1 baada ya bao la mapema la Hugo Ekitike, Messi aliufanya mchezo kuwa salama dakika ya 72 na kupachika bao.
Akizungumza baada ya ushindi huo, Galtier aliwashukuru mashabiki kwa kusherehekea mafanikio ya Messi nchini Qatar, licha ya Argentina kuifunga Ufaransa katika fainali ya Kombe la Dunia.
Galtier amesema; “Asante kwa wafuasi wetu kwa kumkaribisha kwa jinsi walivyomkaribisha. Hiyo ina maana kubwa kwake. Mashabiki wetu pia walimfuata wakati mchezo ulipokuwa mgumu.”
Messi amepona vizuri. Amekuwa na mazoezi machache na sisi sasa. Alionekana mwepesi na mwenye umbo zuri sana. Ni kweli, timu ni tofauti na Messi na bila, pia alifunga bao muhimu kwetu usiku wa leo na sote tunajua kuwa anapenda kufunga mabao, ni aina ya mchezaji anayehitaji mabao. Kocha huyo alisema.
Galtier pia alieleza kwa nini alichagua fomesheni ya 3-4-2-1, akisisitiza umuhimu wa timu yake kuwa na uwezo wa kubadilika huku wakiendeleza uongozi wao kileleni mwa msimamo hadi pointi sita kufuatia kichapo kutoka kwa Lens.
Kocha huyo amesema kuwa ilikuwa kwa mchezo huu, kulingana na jinsi walivyojiandaa alihisi haitafanya kazi kwa jinsi walivyojiandaa. Pia alizungumza na wachezaji wake na wafanyakazi wake kuhusu chaguzi zetu, na wakachukua chaguo tofauti.
Timu ilifanya vizuri sana katika mfumo huo mwanzoni mwa msimu katika michezo mikubwa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa usiku wa jana. Ni muhimu kwa timu kama Paris Saint-Germain, kwa wachezaji wake, na pia, kwake na wafanyakazi kuwa na chaguzi, pamoja na uwezo wa kubadili kutoka mfumo mmoja hadi mwingine.