Greenwood Huyooo Marseille

Winga wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ambaye alikua anakipiga klabu ya Getafe ya nchini Hispania amekaribia kujiunga na klabu ya Olympique Marseille ya nchini Ufaransa.

Olympique Marseille ambayo kwasasa ipo chini ya kocha wa zamani wa Brighton Roberto de Zerbi iko mbioni kukamilisha usajili wa Greenwood ambapo Manchester United ilitanabaisha mapema kumuweka sokoni, Marseille wametoa ofa ya £27 milioni kwajili kupata huduma ya winga huyo.greenwoodKlabu ya Manchester United inahitaji kukamilisha dili hilo mapema ili kuipata kiasi cha fedha ambacho watakitumia katika kuhakikisha na wao wanakamilisha dili la wachezaji wao ambao wanawahitaji sokoni kama beki Mathijjs De Ligt, Joshua Zirkzee, na kiungo Manuel Ugarte.

Olympique Marseille wanahitaji kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao huku kocha De Zerbi akihitaji kua mshindani halisi kwenye ligi kuu ya Ufaransa, Lakini kuirudisha timu hiyo kwenye ligi ya mabingwa ulaya ambapo winga Mason Greenwood ndio amekua chaguo lao la awali kuelekea msimu ujao klabuni hapo.

Acha ujumbe