Paris FC inatarajiwa kumteua kocha Muingereza Liam Rosenior kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kuelekea mwanzo wa msimu mpya, akichukua nafasi ya Antoine Kombouare. Taarifa kutoka RMC Sport zinaeleza kuwa Rosenior yupo mbioni kurejea Ufaransa baada ya kipindi kifupi alichokitumia nchini England.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mazungumzo kati ya Paris FC na Kombouare yalikwama kutokana na tofauti za kifedha. Mchambuzi wa soka Daniel Riolo alisema, “Ni kweli Paris FC ina uwezo wa kifedha, lakini haikuwa tayari kukubaliana na kila kitu, hasa kuhusu madai ya Antoine Kombouare ya kuongezewa fedha. Mazungumzo yalichukua muda mrefu hadi uongozi ukachoka, na sasa yamefikia mwisho.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Riolo aliongeza kuwa Rosenior hakuwa chaguo pekee lililofikiriwa na klabu hiyo, akisema, “Kulikuwa pia na mazungumzo na Walid Regragui. Kulikuwa na mikutano miwili au mitatu, lakini inaonekana Rosenior ndiye aliyechaguliwa kuiongoza Paris FC.”
Antoine Kombouare alijiunga na Paris FC mwishoni mwa Februari 2026 na kufanikiwa kuiwezesha timu hiyo kumaliza msimu katika nafasi za katikati ya msimamo wa ligi. Hivi karibuni alikuwa amesisitiza kuwa angerudi kuiongoza timu wakati wa kuanza maandalizi ya msimu mpya.
Hata hivyo, taarifa za sasa zinaonyesha kuwa uongozi wa Paris FC umeamua kwenda na mwelekeo tofauti kwa ajili ya msimu ujao, huku Liam Rosenior akitarajiwa kutambulishwa rasmi kama kocha mpya atakayeiongoza timu hiyo katika kampeni za msimu wa 2026/27.


