Kocha wa klabu ya PSG Luis Enrique amesema kua winga wake raia wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele atarejea kwenye kiwango chake bora, Hii ni kutokana na maneno ambayo anatupiwa mchezaji huyo.
Luis Enrique ameonesha kumtetea kwa mara nyingine mchezaji wake huyo ambaye watu wengi wanahoji ubora wake mpaka sasa, Kwani mchezaji huyo hajafanikiwa kuonesha cheche zake mpaka sasa ndani ya PSG.Winga huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona amekua akionesha kiwango cha chini tangu atue klabuni hapo, Lakini kocha wake amesema anafurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo mpaka sasa.
Kocha wake ameeleza kua anafurahishwa na ambacho Dembele anakifanya mpaka sasa na anaamini namba zake zitapanda, Kama kufunga mabao na vilevile kocha huyo anaamini mchezaji huyo hatakiwi kupewa presha kwani anaamini atarejesha makali yake.Maneno ya kocha Luis Enrique yanaonekana kulenga kumtengenezea Dembele saikolojia nzuri na kumrudisha mchezoni, Kwani mashabiki wa klabu hiyo wanaonekana kutoridhishwa na kiwango cha winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa.