Mbappe Awaaga Wachezaji Wenzake

Mshambuliaji wa klabu ya PSG Kylian Mbappe inaelezwa mapema asubuhi ya leo amewaaga wachezaji wenzake na kuwaeleza ataondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mwanzoni mwa wiki hii taarifa zilitoka kua Mbappe ameueleza uongozi wa klabu ya PSG kua ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba wake utafikia ukomo.mbappeInafahamika staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu, Hivo kupitia taarifa ya kuondoka kwake mwishoni mwa msimu ni wazi mshambuliaji huyo ataondoka bure ndani ya klabu hiyo.

Taarifa nyingi zinaeleza kua nyota huyo anafikiria zaidi klabu moja kichwani kwake na ambayo imefanya majaribio kadhaa ya kumsajili, Lakini ikashindikana na sio klabu nyingine ni mabingwa mara nyingi zaidi wa ulaya klabu ya Real Madrid.mbappeKiu kubwa ya mshambuliaji Kylian Mbappe ni kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya ambapo anaamini kupitia klabu ya Real Madrid anaweza kutimiza ndoto hiyo ambayo amekua akiiota kwa muda mrefu sasa.

Acha ujumbe