Mshambuliaji wa klabu ya PSG Kylian Mbappe amefanikiwa kuipita rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa klabu ya PSG ya nguli Edson Cavani na kuweka ya kwake baada ya kufunga goli la 201 hapo jana.
Kylian Mbappe ambaye alifanikiwa kuvunja rekodi ya Cavani katika mchezo uliomalizika dhidi ya klabu ya Olympique Marseille na kufikisha mabao 200 hivo kua sawa na Cavani, Lakini hapo jana nyota huyo amefanikiwa kuweka ya kwake.Mchezaji huyo ambaye alijiunga na klabu ya PSG mwaka 2017 kabla ya kujiunga kwa mkataba wa jumla ndani ya klabu hiyo mwaka 2018 kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 180, Kuanzia hapo mchezaji huyo amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo.
Mbappe alifanikiwa kuweka rekodi jana baada ya kufunga bao katika dakika za nyongeza katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya klabu ya Nantes,Mshambuliaji huyo kwasasa anafanikiwa kuweka rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo akiwa na miaka 24 tu.Mshambuliaji Mbappe jana baada ya kufanikiwa kufunga bao katika mchezo huo na kufikisha mabao 18 katika ligi kuu ya Ufaransa, Huku akiendelea kuongoza kwenye mbio za kiatu cha ufungaji wa ligi kuu ya Ufaransa na akifanikiwa kubeba kiatu hicho itakua mara ya tatu mfululizo.