Mechi ya Marseille VS Lyon Iliahirishwa Baada ya Basi la Timu Kuvamiwa

Mechi ya Lyon ya Ligue 1 dhidi ya Marseille iliahirishwa baada ya basi la timu hiyo kushambuliwa.

 

Meneja Fabio Grosso alipata jeraha la kichwa baada ya basi hilo kuripotiwa kushambuliwa na mashabiki walioripotiwa kurusha makombora lilipokuwa likielekea Stade Velodrome.

Cheza Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Kulingana na ripoti zilizoenea, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Italia Grosso alipigwa na vipande vya kioo na alihitaji matibabu huku uso wake ukivuja damu nyingi.

Rais wa Marseille Pablo Longoria aliiambia Prime Video Sport: “Haikubaliki. Ninasema kwa dhati, lazima tuzuie kile kilichotokea kwa Fabio Grosso hakikubaliki kabisa. Ni jambo ambalo haliwezi kutokea katika soka.”

Ni wazembe tu. Kuharibu karamu, katika uwanja wenye watu 65,000 kwa sababu ya uzembe. Nina hasira. Hasa kwa sababu haina nafasi katika soka, au katika jamii. Alisema rais huyo.

Pambano kati ya Lyon iliyo mkiani na Marseille iliyo katika nafasi ya 10 lilipaswa kuanza saa 4:45 usiku wa jana

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Tayari mashabiki walikuwa uwanjani wakati tangazo lilipotolewa kuwa mchezo huo umeahirishwa.

Klabu inamtakia ahueni ya haraka kocha wa Lyon, Fabio Grosso na inalaani vikali tabia hiyo ya ukatili ambayo haina nafasi katika ulimwengu wa soka na katika jamii.

Lyon imesalia bila ushindi kwenye Ligue 1, huku uamuzi wa kumbadilisha Laurent Blanc na kumuingiza Grosso bado haujazaa matunda kwa mabingwa hao mara saba.

Meneja wa Marseille, Genaro Gattuso pia yuko kwenye shinikizo ndani ya Marseille baada ya kupoteza michezo mitatu kati ya minne iliyopita.

Acha ujumbe