Staa wa klabu ya PSG Lionel Messi ameisaidia klabu yake kuweza kupata matokeo katika mchezo dhidi ya Lille baada ya kufunga bao la jioni kabisa kupitia mpira wa adhabu.

Klabu ya PSG ilikua na wakati mgumu leo dhidi ya Lille kwani mpka dakika ya 70 ya mchezo klabu hiyo ilikua nyuma kwa mabao matatu kwa mawili kabla ya Mbappe kusawazisha mnamo dakika ya 87, Lionel Messi yeye alipigilia msumari kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 95 kupitia mpira wa adhabu.MessiKlabu ya PSG baada ya matokeo ya leo inaendelea kushika usukani wa ligi kuu ya Ufaransa baada ya kufikisha jumla ya alama 57 wakifutaiwa na klabu ya Olympique Marseille wenye jumla ya alama 49, Hivo baada ya ushindi huo wanaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa walikutana na mchezo wenye ushindani mkubwa sana kwani klabu ya Lille ilifanikiwa kuonesha ubora mkubwa, Huku PSG wao wakiwa wanafanya kazi ya kusawazisha mabao kabla ya Messi kuhakikisha PSG wanaondoka na alama tatu muhimu.MessiKatika mchezo huo mbali na Lionel Messi kufunga bao dakika za lala salama lakini pia nyota mwingine ndani ya timu Kylian Mbappe alikua na msaada mkubwa katika mchezo huo, Kwani katika ushindi wa mabao matano walioupata PSG  mchezaji huyo ameweza kufunga mabao matatu.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa